Katibu Mkuu Mhandisi Samamba akutana na ujumbe kutoka Marekani

DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba, ameupokea ujumbe wa Serikali ya Marekani kupitia Ubalozi wake nchini na kufanya kikao kifupi cha utambulisho ambapo ujumbe huo umeeleza kusudio la kufika wizarani.
Akizungumza katika kikao hicho kifupi, kilichofanyika leo Julai 16, 2024, Mhandisi Samamba ameueleza ujumbe huo kuhusu mpango wa Wizara kuhuisha Mpango Mkakati wake ili kuiwezesha kukidhi matakwa ya dhamira yake ya kuendeleza madini muhimu.
Sambamba na utayari wa Wizara ya Madini kushirikiana na Marekani katika uendelezaji wa madini hayo na kuongeza kwamba, Wizara Iko tayari kubadilishana taarifa za msingi zitakazowezesha kusudio la ushirikiano huo.

"Mkitoka hapa mtapata nafasi ya kukutana na taasisi zetu za GST, STAMICO na Tume ya Madini ambao watatoa mawasilisho yatayowasaidia ninyi kupata taarifa muhimu. Pia, STAMICO wanayo maeneo ambayo wangependa kushirikiana kuyaendeleza Kwa hivyo mtasikia mengi kutoka kwao," amesema Mhandisi Samamba.
Naye, Meneja Mipango wa Idara ya Rasilimali Nishati na Madini kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Bw. Evan McGlaughlin

amesema nchi hiyo imelenga kushirikiana na Tanzania katika maeneo kadhaa ikiwemo kuboresha mkakati wa kuendeleza madini mkakati, ushirikiano katika masuala ya jiosayansi na kuwajengea uwezo wataalam wa ndani.
Pia, ameishukuru Wizara kwa kuupokea ujumbe huo na kuukutanisha na taasisi zake utakaowezesha kuanzisha ushirikiano baada ya kuwa na majadiliano kwa takriban kipindi cha mwaka mmoja nyuma

Itakumbukwa Tanzania inajiandaa vilivyo katika uendekezaji wa madini mkakati hususan kupitia Vision 2030: Madini ni Maisha& Utajiri katika kipindi hiki ambacho kuna mahitaji makubwa ya madini hayo duniani.
Madini mkakati yanayotumika kutengenezea bidhaa mbalimbali za teknolojia ikiwemo za betri za magari ya umeme, betri za simu na vizuia joto.

Madini hayo ni kama kinywe, nikeli, lithium, manganese, kolbati na mengine ambayo Tanzania imebarikiwa kuwa nayo.

#InvestInTanzaniaMiningSector

#Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news