DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ametoa wito kwa wawekezaji kutoka nchini Urusi waje kuwekeza nchini Tanzania kwenye Sekta ya Sanaa na Michezo kwa kuwa Tanzania imeshaweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta hizo na Sekta nyingine.

Amesema, Tanzania na Urusi zina ushirikiano katika Sekta ya Biashara ambapo bidhaa za Tanzania zenye thamani ya dola za Marekani milioni 6.4 zinauzwa Urusi na bidhaa za Urusi za thamani ya Dola za Marekani milioni 179 nchini Tanzania hivyo Watanzania wanayo nafasi ya kujifunza zaidi kutoka katika nchi hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetsyan amesema,nchi hiyo inafurahishwa na ushirikiano uliopo miongoni mwa nchi hizo, akieleza kuwa nchi hiyo ipo tayari kuongeza ushirikiano katika maneno mengi zaidi hasa teknolojia.