DAR-Uongozi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umetangaza kuwa, utamchukulia hatua za kinidhamu Kibu Denis Prosper kwa kushindwa kuripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024|2025.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na klabu hiyo akifafanua, Kibu amekuwa akitoa sababu kadha wa kadha zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini.