DAR-Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana, ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.
.jpeg)
Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa, chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila vitakapohitajika. “Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.”