Kituo cha Afya cha Gumanga chafanya upasuaji mkubwa wa kwanza

SINGIDA-Kituo cha Afya cha Gumanga kilichopo kata ya Gumanga Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kimefanikiwa kufanya upasuajia mkubwa wa kwanza wa dharura kwa mama mjamzito toka kufunguliwa kwake.
Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Mganga Mkuu wilaya ya Mkalama Dkt. Solomon Michael amesema upasuaji huo umefanyika Julai 01,2024 chini ya madaktari wawili wakisaidiwa na wauguzi pamoja na mtalaamu wa uzingizi.

"Kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa hapa Gumanga toka tuanzishe huduma hizi za upasuaji. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu.Mtoto aliyezaliwa ni wakike na uzito wa kilo 3.1, hali ya mama na mtoto inaendelea vizuri," aliongeza Dkt. Michael.

Kwa mujibu wa Dkt.Solomon Michael amesema,mjamzito huyo amefika kituoni hapo siku ya Jumatatu ya Julai 1,2024 muda wa asubuhi na kufanyiwa upasuaji muda wa saa moja usiku. Aidha, timu ya wataalamu iliyoongoza zoezi hilo ni Dkt. Sira Laurent Kisamhara, akisaidiwa na Dkt. Lazaro Chambo, wauguzi wakiwa Seleman Mwalukasa, Faraja Shadrack, na Richard Sopeter mtaalamu wa usingzi pamoja a mtaalam wa Maabara Patric Sanga.

Kituo cha afya cha Gumanga kinakuwa ni kituo cha tatu cha serikali wilayani Mkalama kinachotoa huduma za upasuaji, vingine ni Hosipitali ya Wilaya ya Mkalama pamoja na kituo cha Afya cha Kinyambuli.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news