Kwa orodha hii kusalimika ni vigumu, DCEA inaanza na hawa

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) imesema imekamilisha Kanzidata ya watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ndani na nje ya Tanzania na tayari imeanza uchunguzi kwa hatua za kisheria.
Hayo yamesemwa leo Julai 17,2024 jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo wakati akizungumza na wanahabari kupitia hafla fupi ambayo imejumuisha tukio la kuwapa tuzo wadau mbalimbali.


"Kwa sasa pia tumekamilisha Kanzidata. Data base ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na tumeanza uchunguzi juu ya watu hao.

"Wengi wamebainika wapo ndani ya nchi na wengine nje ya nchi. Baadhi yao wana biashara nyingine halali, lakini wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kufanya utakatishaji.

"Mamlaka inatoa wito kwao kuachana mara moja na biashara hiyo na kujikita kwenye biashara halali. Kwani uchunguzi dhidi yao unaendelea."

Kamishna Jenerali Lyimo amesema kuwa, kwa muda mrefu walikuwa wanaandaa Kanzidata ya wale wanaoshiriki na wanaofadhili biashara ya dawa za kulevya.


"Na hii Kanzidata tayari tumeshaikamilisha, kwa hiyo tunayo sasa hivi orodha ya watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya waliopo ndani ya nchi na walioko nje ya nchi za nje.

"Na hii Kanzidata tumebaini pia baadhi ya watu wamejificha kwenye biashara nyingine halali. Lakini, nyuma yake wanafadhili biashara ya dawa za kulevya.

"Na wao kwenye ule mnyororo wa biashara za kulevya hawaonekani, sasa tumeanza uchunguzi madhubuti kuhakikisha tunawabaini wale wote ambao wanajihusisha na kufadhili biashara ya dawa za kulevya hatua kali zitachukukuliwa dhidi yao.


"Kwa hiyo nitoe wito kuanzia muda huu wote waachane na biashara ya dawa za kulevya na wajikite kwenye biashara halali ambazo wanazifanya.

"Na kuanzia sasa hivi wale watakaoacha hatutaangaika nao, lakini kadri uchunguzi unavyoendelea wale wote watakaobainika wanajihusisha na kufadhili biashara ya dawa za kulevya na kutakatisha fedha kwenye biashara nyingine halali hatua za kisheria zitachukukuliwa dhidi yao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news