MWANZA-Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawasaka wananchi waliozusha taarifa za kupigwa hadi kufariki mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mlimani iliyopo Kata ya Bugarika wilayani Nyamagana, Leonia Amiri (16).
Uzushi huo ulitokea Julai 11,2024 ikidaiwa mwanafunzi huyo alipigwa na mwalimu hadi kumsababishia kifo, hatua iliyopelekea wananchi kukusanyika shuleni hapo kwa fujo, akiwemo mama mzazi wa mwanafunzi, Christina Joshua (35) ambaye tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Wilbrod Mutafungwa ametembelea kata hiyo kuwapatia wananchi elimu ya ulinzi na usalama huku akiwataka kuifanyia uchunguzi taarifa yoyote wanayopokea, badala ya kufanya uzushi unaoweza kupelekea uvunjifu wa amani katika jamii.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo