Magazeti leo Julai 15,2024

TANGA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema linamshikilia Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Kombo Twaha Mbwana (29) kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zacharia Bernard ametoa taarifa hiyo Julai 14,2024.
"Jeshi la Polisi linamshikilia Kombo Twaha Mbwana (29) mkazi wa Kwamsala Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo ameyatenda katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi, upelelezi wa matukio hayo umefikia hatua nzuri na wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani."






















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news