Magazeti leo Julai 17,2024

LUDEWA-Wanakijiji 3,149 wa Kijiji cha Mundindi kilichopo Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wametengeneza historia ya kipekee baada ya Serikali ya kijiji hicho kuwakatia bima ya afya wote ili waweze kupata huduma ya afya bila kikwazo cha fedha.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kulipa fidia shilingi bilioni 15 ili kupisha miradi ya Liganga na Mchuchuma ambapo kijiji hicho kilikuwa na eneo katika eneo la mradi huo na kukiwezesha kupata fidia ya shilingi milioni 464.
Kati ya fedha hizo, na shilingi milioni 400 kijiji kiliamua kununua hati fungani katika moja ya taasisi ya kifedha hapa nchini.

Hayo yamesemwa Julai 12, 2024 na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mundindi, Sapi Mlelwa wakati wa hafla ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya wananchi hao, iliyofanyika kijijini hapo.

Amesema, kiasi hicho cha shilingi milioni 400 walichonunua bondi ya hati fungani, kinawawezesha kijiji hicho chenye kaya 524, kupata gawio la shilingi milioni 41 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano.

Amesema katika gawio la kwanza, wanakijiji walikubaliana kulipiana bima ya afya ambayo thamani yake ni shilingi milioni 12.9.














Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news