DODOMA-Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeongeza kasi ya kushughulikia malalamiko ya uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Ni kutokana na upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya uchunguzi ambapo kwa mwaka 2022/23 tume hiyo ilikuwa ikishughulikia jumla ya malalamiko 1,524 ambapo ilihitimisha jumla ya malalamiko 789 na kufanya malalamiko yaliyoendelea kuanzia Julai 1, 2023 kuwa 885.
Hayo yamebainishwa Julai 19,2024 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti mbalimbali za chunguzi zilizofanywa na tume kwa Mwaka wa 2023/24.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo