KIAMBU-Wizara ya Afya nchini Kenya imetoa tahadhari baada ya trela lililobeba sumu kali aina ya Sodium Cyanide kuanguka katika eneo la Kambembe huko Rironi katika Kaunti ya Kiambu.Sodium Cyanide inatajwa kuwa mojawapo ya sumu kali zaidi duniani, kutokana na uwezo wake wa kusababisha kifo mara moja.
Ina rangi nyeupe, na huweza kuchanganyika kwa wepesi na maji na vyuma pia, jambo linaloifanya kuwa hatari.
Kwa mujibu wa Taifa Leo, taarifa kutoka kwa Katibu wa wizara hiyo,Mary Muthoni inasema kwamba umma unatahadharishwa dhidi ya kusogelea eneo hilo la mkasa, kwa sababu kemikali hiyo ni hatari mno kiasi cha kusababisha kifo iwapo mhusika anatagusana nayo kwa wingi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo