Magazeti leo Julai 28,2024

SINGIDA-Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameipongeza Kampuni ya AL FRADAWS Investment Company Limited kutoka Jordan ambayo ni wawekezaji katika uzalishaji wa mbegu mbalimbali mkoani Singida kwa kuja na suluhisho katika upatikanaji wa maji mkoani humo kupitia Teknolojia ya Pivot Irrigation System.Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa yenye changamoto ya vyanzo vya maji vya uhakika na upatikanaji maji chini ya ardhi.
Akizungumza wakati alipotembelea kampuni iliyopo Kijiji cha Choda wilayani Ikungi tarehe 27 Julai, 2024 Waziri Aweso amesema, teknolojia ambayo inatumiwa na Kampuni ya FRODAWS ni nzuri kwa kuwa inatoa majibu ya uhakika katika utambuzi wa maeneo yenye maji kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji.

Lengo la ziara hiyo ambayo imehusisha utafiti wa vitendo kwa njia ya anga kwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mji wa Kiomboi mjini Singida ni kuona namna gani teknolojia hiyo inavyoweza kutumika katika maeneo mbalimbali nchini ili kutatua tatizo la maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news