DAR-"Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuufahamisha umma kuwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/24, imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.67 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 28.30.
"Makusanyo haya ni ongezeko la asilimia 14.50 ikilinganishwa na makusanyo ya Shilingi Trilioni 24.14 katika Mwaka wa Fedha uliopita, 2022/23.
"Katika kipindi cha robo mwaka ya nne yaani Aprili - Juni, 2024, TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 7.09, sawa na ufanisi wa asilimia 99.46 ya lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 7.13.
"Makusanyo haya ni ongezeko la asilimia 24 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 5.72 kilichokusanywa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha uliopita 2022/23;