Marekani, Ujerumani vinara uuzaji silaha Israel

NA DIRAMAKINI

SERIKALI za Marekani na Ujerumani zimedaiwa kuhusika na usambazaji wa asilimia 99 ya silaha za moto ambazo ziliagizwa na Israel ili kutekeleza mapigano huko Gaza kati ya mwaka 2019 na 2023.
Bomu la MK-84 ambalo linatajwa kuwa na uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa katika miundombinu mbalimbali kwa muda mfupi.(PICHA NA JASON R. ZALASKY/AFP).

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (The Stockholm International Peace Research Institute-SIPRI).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 69 ya silaha ilitoka nchini Marekani na asilimia nyingine 30 ilitoka nchini Ujerumani.

Oktoba 7, mwaaka jana kabla ya kuanza operesheni ya Al-Aqsa na kufuatiwa na mashambulizi katika ukanda huo wa Gaza,Marekani ilikuwa ikiitumia Israel silaha zenye thamani ya wastani wa dola bilioni tatu kila mwaka.

Aidha,katika miaka mitano iliyopita, Israel ulipokea asilimia 3.6 ya silaha zote zinazouzwa nje na Marekani.

Vile vile,SIPRI imebainisha kuwa, Marekani ilituma maelfu ya silaha na makombora ya kisasa kwa utawala wa Israel kufikia mwishoni mwa mwaka jana.

Aidha,Ujerumani ilitoa leseni ya kuiuzia Israel silaha zenye thamani ya Euro milioni 326.5.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, ni Euro milioni 38.5 tu za mauzo ya kijeshi kwa utawala wa Israel ndizo ziliidhinishwa na serikali ya Ujerumani.

Hata hivyo, baada ya Oktoba 7, 2023, tangu utawala huo uanzishe mashambulizi dhidi ya watu wa Palestina huko Ukanda wa Gaza, idadi hii imeongezeka zaidi.(NA)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news