Mhandisi Seff:Fanyeni kazi kwa bidii kulinda taswira ya TARURA

KIGOMA-Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kulinda taswira nzuri ya wakala huo.Rai hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na watumishi wa TARURA mkoa wa Kigoma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
Mhandisi Seff amesema kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa kutekeleza majukumu ya Wakala na kuleta tija katika malengo na kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa ufanisi mkubwa.

Aidha, Mtendaji Mkuu huyo amewapongeza wafanyakazi hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwataka wasibweteke.
Wakati huo huo Mhandisi Seff alitembelea na kukagua barabara za Manispaa ya Kigoma -Ujiji na kumtaka Meneja wa TARURA Mkoa kuhakikisha wanazifanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara zilizojengwa ili kuzilinda na kuzifanya zidumu kwa muda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news