Mheshimiwa Katimba awahimiza waumini wa Kanisa la Anglican kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

KIGOMA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba ametoa wito kwa waumini wa Kanisa la Anglican nchini kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata fursa ya kuchagua viongozi bora watakaoliletea taifa maendeleo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akipokea zawadi ya Naibu Waziri Mkuu na ha Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko kutoka kwa Baba Askofu Emanuel Charles Bwata wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu la Anglican wakati wa ibada ya harambee maalumu ya ujenzi wa kanisa hilo lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.

Mhe. Katimba ametoa wito huo wakati akimuwakilisha Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko kwenye ibada ya harambee maalumu ya ujenzi wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akipokea zawadi yake kutoka kwa Baba Askofu Emanuel Charles Bwata wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu la Anglican wakati wa ibada ya harambee maalumu ya ujenzi wa kanisa hilo lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akishiriki ibada ya harambee maalumu ya ujenzi wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu la Anglican lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.

“Sote tunafahamu Mhe. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezindua zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura hapa mkoani Kigoma, hivyo niwakumbushe kujiandikisha na kuboresha taarifa zenu ili kumuunga mkono Mhe. Rais kwa kuchagua viongozi watakaoshirikiana nae kuleta maendeleo nchini,” Mhe. Katimba amesisitiza.

Mhe. Katimba amesema zoezi la kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura mkoani Kigoma litakuwa la siku saba hivyo wananchi wajitokeze mapema kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili kupata sifa ya kushiriki uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.

Sanjari na hilo, Mhe. Katimba amewasilisha mchango wa shilingi milioni 20 uliotolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko kuchangia ujenzi wa wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akifurahia jambo wakati wa ibada ya harambee maalumu ya ujenzi wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu la Anglican lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.

Akizungumzia ushiriki wa waumini katika maboresho ya Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Baba Askofu Emanuel Charles Bwata amemhakikishia Mhe. Katimba kuwa, kanisa linawaamasisha waumini kujiandikisha na kuongeza kuwa binafsi yeye alishaanza kuwahamasisha kabla ya Mhe. Waziri Mkuu kuzindua rasmi zoezi hilo mkoani Kigoma.

Aidha, Baba Askofu Emanuel Charles Bwata amemshukuru Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko kwa kutoa mchango wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu la Kasulu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akiwa katika picha ya pamoja na Baba Askofu Emanuel Charles Bwata wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu la Anglican na viongozi wengine, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya harambee maalumu ya ujenzi wa kanisa hilo lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.

Jumla ya milioni 134,134,200 zilipatikana katika ibada hiyo ya harambee maalumu ya ujenzi wa Kanisa Kuu la Andrea Mtakatifu la Uaskofu lililopo Kasulu Dayosisi ya Western Tanganyika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news