Mheshimiwa Leila atembelea banda la OUT maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu kisiwani Pemba

ZANZIBAR-Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali-Zanzibar, Mh. Lela Muhamed Mussa, ametembelea Banda la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kujionea shughuli mbalimbali za chuo zinazoenezwa katika Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu yanayofanyika katika Viwanja vya Gombani mjini Chakechake, Pemba.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo Mh. Lela, amewahimiza wakazi wa kisiwa hiki kuchangamkia fursa mbalimbali zilizosogezwa katika maonesho hayo kwani huduma zingine ingewalazimu kuzifuata sehemu nyingine.
Aidha, Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dkt. Adam Namamba, amesema maonyesho haya yamekuwa ni fursa kubwa kwa chuo hiki kueneza huduma zake kwa wakazi wa Pemba ambao wamefika kwa wingi kujua fursa zitolewazo na chuo hiki.

Aliendelea kusema kuwa, chuo hiki kimekuwa na Kituo cha Uratibu katika Kisiwa hiki kwa miaka mingi hivyo maonesho haya yamesaidia kukifikisha zaidi kwa jamii ambayo imefika kwa wingi bandani kupata huduma mbalimbali.
Aidha, mwamko mkubwa ulioonyeshwa na wakazi wa kisiwa hiki kwa kutamani kupata fursa ya udhamini wa program ya msingi kwa watoto wa kike lakini pia fursa ya mafunzo ya TEHAMA kwa kundi la watu wenye mahitaji maalum umemfanya kuona kuna umuhimu mkubwa wa kukuza masoko katika eneo hili.

Maonesho ya Wiki ya Elimu ya Juu yanayoendelea kisiwani Pemba yameratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar ambapo yameanza kurindima Julai 24, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Julai 28, 2024 katika Viwanja vya Gombani vilivyopo Chakechake Kisiwani Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news