Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amedhamiria kuendelea kufikisha huduma za jamii kote nchini-Waziri Mkuu

LINDI-Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa leo Julai 3, 2024 amezungumza na wakazi wa Kijiji cha Mmawa kilichopo katika kata ya Nandagala, Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na Wakazi hao Mheshimiwa Majaliwa amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kufikisha huduma za jamii ikiwemo afya, maji, umeme na elimu katika maeneo yote nchini.
“Kwa mfano katika Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea tuna mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 119, kwa mradi huu maeneo mengi hapa yatapata huduma ya maji. Rais Dkt. Samia pia aliamua kununua mitambo ya kuchimbia visima vya maji lengo ni kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwenye maeneo yetu.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka maafisa kilimo nchini kuweka mpango wa kuwahamasisha na kuwasimamia vijana kuingia katika kilimo cha bustani kwenye maeneo ya mabonde yanayofaa kwa kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news