Mheshimiwa Ridhiwani ateta na wanawake wanaofanya biashara ya kuuza vyakula

PWANI-Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze,Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayathamini makundi mbalimbali nchini ikiwemo wanawake wajasiriamali.
Mheshimiwa Ridhiwani ameyasema hayo baada ya kukutana na kundi la wanawake wanaofanya biashara ya kuuza vyakula.

"Katika kutekeleza majukumu yeyote, kundi muhimu ni hili la hawa tunaowatumikia. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imewezesha sio tu mazingira ya kufanya biashara, lakini pia kuwajengea maeneo mazuri ya kufanya biashara, mikopo ya asilimia 10 na ile inayotolewa na halmashauri.
"Halmashauri ya Chalinze imekopesha zaidi ya shilingi milioni 850, zimetolewa kwa wakina mama wanaofanya biashara katika halmashauri hii,"amesisitiza Mheshimiwa Ridhiwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news