SINGIDA-Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ndugu Godfrey Mzava amewataka wananchi wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2024.

“Uchaguzi upo tayari mlangoni, tujitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi huu muhimu wa kuchagua viongozi wetu. Tukio la kupiga kura halitachukua muda mrefu, twendeni tukapige kura. Lakini pia tulinde amani na umoja wakati wa uchaguzi,” Mzava

“Tuchukue wajibu wa kulinda mazingira yetu, nimepita shule ya Mkalama One nimeona kazi nzuri, nimeona mmeanzisha mradi wa mazingira. Tukifanya hivi tutakuwa vinara katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira.”

“Tumepita tumeona kazi kubwa imefanyika wilayani Mkalama, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu anatoa fedha lengo likiwa ni kuona wananchi wanapata huduma nzuri."
Mbio za Mwenge 2024 wilayani Mkalama zimezindua mradi mmoja na kuweka jiwe la msingi katika miradi miwili ambapo miradi yote ina thamani ya jumla ya shilingi 2,067,623,126.00 na umetembelea program 8 ambazo ni Lishe, Mazingira, Rushwa, Dawa za kulevya, VVU/UKIMWI, Malaria, Elimu kwa Mpiga Kura na Kongamano la Vijana.