Mkurugenzi Mkuu wa TAEC ahitimisha ziara Kanda ya Ziwa iliyomkutanisha na wadau mbalimbali

MWANZA-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof.Najat Kassim Mohammed amehitimisha ziara yake ya kutembelea ofisi za Kanda ya Ziwa kuzungumza na wadau wanaoshirikiana na TAEC.
Sambamba na kuzungumza na wafanyakazi wa TAEC ili kujua mafanikio na changamoto wanazopitia katika kutekeleza majukumu yao.

Prof. Najat ametembelea vituo sita ambavyo ni Kituo cha TARI-Ukiliguru, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Uwanja wa Ndege jijini Mwanza, Bandari ya Mwanza, Ofisi ya Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa iliyopo Nyegezi jijini Mwanza pamoja na Ofisi ya TAEC mpakani Sirari mkoani Mara.
Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Sirari mkoani Mara,Prof. Najat amesema, ziara yake imelenga kukutana na taasisi ambazo zina ushirikiano na TAEC ili kujitambulisha pamoja na kuona maeneo ya kuongeza ushirikiano ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC).
Aidha, Prof. Najat ametumia nafasi hiyo kuzungumza na wafanyakazi wa Kanda ya Ziwa ambapo amefahamu utendaji wao wa kazi sambamba na kuahidi kutatua changamoto zinazowakabili ili kuleta ufanisi eneo la kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news