Momba yaanza kuchimba madini ya Sodalite,waipongeza Wizara ya Madini

SONGWE-Wizara ya Madini imeendelea na Kliniki ya Madini katika Mkoa wa Songwe katika ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji kwa lengo la kupokea kero na changamoto za wachimbaji wadogo wa madini.
Julai 4 , 2024 Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wilayani Momba alikutana na wachimbaji wadogo wa madini na kuzungumza nao kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.
Akiwa katika kijiji cha Chindi , Kata ya Msangano, Naibu Waziri Dkt. Kiruswa alitembelea Mgodi wa mchimbaji mdogo wa Madini ya Sodalite na kupokea taarifa ya maendeleo ambapo mpaka sasa mgodi huo umezalisha kiasi cha tani 50 huku changamoto kubwa ikibainishwa ni ukosefu wa mtaji , kutokuwepo kwa mthaminishaji wa madini katika eneo la uzalishaji, soko la uhakika na ubovu wa miundombinu.

Sambamba na madini hayo , Dkt.Kiruswa alikutana na wachimbaji wa Gesi ya Helium na Madini ya Chumvi ambapo katika miradi hiyo aliwapongeza kwa juhudi mbalimbali wanazofanya katika kuendeleza miradi hiyo ambayo ni muhimu katika sekta ya uchumi nchini.
Naye , mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalee aliishukuru Wizara ya Madini kwa kuanza kuendesha kliniki ya madini katika mkoa wa Songwe na kupokea changamoto mbalimbali ambazo zikitatuliwa itakuwa faida kubwa kwa wachimbaji wa mkoa huo na kuendeleza sekta ya madini mkoani wilayani Momba.

Julai 4, 2024,Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amehitimisha ziara yake maalum ya Kiliniki ya madini mkoani Songwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news