Mtendaji jela miaka mitatu kwa kujinufaisha na fedha za wanakijiji

KAGERA-Mahakama ya Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imemhukumu, Bw. Florian Kaizilege Method adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela.
Adhabu hiyo imetolewa baada ya kuthibitika kosa la rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Mshtakiwa imedaiwa kwa makusudi alijipatia manufaa isivyostahili kiasi cha shilingi 1,625,000 alizozikusanya kutoka kwa wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Bwenkoma wilayani Missenyi.

Aidha,Mahakama imeamuru mshtakiwa arejeshe fedha zote shilingi 1,625, 000 kwa mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa taratibu za ujenzi ofisi ya Kijiji cha Bwenkoma.

Hukumu dhidi ya Florian Kaizelege Method imeamriwa katika shauri la Rushwa Na. 21076/2024 la Julai 26, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Missenyi, Mheshimiwa Yohana Muyombo mbele ya waendesha mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Daudi Jacob Oringa na Sospeter Joseph.

Mshtakiwa ameenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news