Mtwara Vijijini wakati ukifika pigeni chini,twendeni na CCM-Nchimbi

MTWARA-Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi akiambatana na Wajumbe wa Sektarieti ameendelea na ziara yake mikoa miwili ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara leo Julai 29,2024 amesalimia na kuzungumza na wananchi wa Jimbo la Mtwara Vijijini Kata ya Mpapura ambalo liko upinzani
Balozi Nchimbi amesema, pamoja na kwamba jimbo hili liko upinzani, lakini utekelezaji wa Ilani ni wa kiwango cha juu.

"Kwani tumeweka Kaimu MbungeMheshimiwa Chikota anayefanya shughuli hapa,hakika kazi imefanyika nafikiri mmeona sasa kazi kwenu wakati ukifika ibidi mbadilike, kwani mnapata maendeleo,lakini hamna wa kumhoji pamoja na yote CCM inawafanyia mambo makubwa tumeyasikia hapa, wenyewe sasa wakati ukifika pigeni chini wasiobadilika kichagueni Chama Cha Mapinduzi."
Mwisho amewaasa wananchi kuendelea kutunza na kulinda asitokee mtu akawadanganya watu kuhusu kuharibu amani tuliyonayo huku akichangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi ya chama Wilaya Mtwara Vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news