Mwandumbya aridhishwa na mikakati ya Wizara ya Fedha na taasisi zake katika kuelimi­sha umma Maonesho ya Sabasaba

NA PETER HAULE

NAIBu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya ametembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya wizara na taasisi zake.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (katikati), akitembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na Taasisi zake. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Kitengo hicho, Bw. Ramadhani Kissimba.

Bw. Mwandumbya alisema kuwa Wizara ya Fedha ni Wizara muhimu katika kuchochea maendeleo ya mchi hivyo ni muhimu elimu ikatolewa kwa usahihi na ufanisi ili watanzania waweze kuelewa majukumu ya Wizara na Taasisi zake.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kulia), akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na Taasisi zake. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na Kushoto ni Mwandishi Mwendesha Ofisi wa Kitengo hicho, Bi. Masia Msuya.

Amesema kuwa,maonesho hayo ambayo Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa pamoja zinatoa nafasi kwa watanzania kupata elimu kwa urahisi kuhusu Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kulia), akipewa maelezo kuhusu Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT – AMIS) namna unavyowahudumia wateja wake na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Rahim Mwanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akohojiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (kushoto) katika kipindi maalumu cha Sabasaba cha Hazina TV baada ya kutembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Eliakim Maswi (kushoto), akihoji masuala ya ununuzi wa vifaa vya Serikali alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (kushoto), baada ya kufanya mahojiano maalumu ya kipindi cha Hazina TV kuhusu Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, ambapo aliipongeza Wizara na Serikali kwa ujumla kwa namna inavyosimamia masuala ya fedha na uchumi.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dkt. Samwel Werema (kulia), akitoa ushauri katika masuala ya tafiti za maendeleo kwa Maafisa wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) alipotembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, yanayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024. Wa pili kulia ni Makamu Mkuu Taaluma wa Chuo hicho, Prof. Provident Dimoso.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa sekta ya Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu ya fedha kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya La Miriam Morogoro, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa sita kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).

Bw. Mwandumbya amewataka Wananchi kutembelea Banda la Wizara hiyo ili wapate elimu na huduma za kibenki, mifuko ya dhamana ya uwekezaji, Sera, masuala ya sekta ya fedha, usuluhishi wa masuala ya kodi, vyuo vya elimu ya juu, ununuzi na ugavi, pemsheni na mirathi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news