DAR-Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba ameweka wazi mambo mazito kuhusu kuibuka kwa huduma nyingi za kiroho hapa nchini huku akibainisha kuwa,shambani mwa Bwana kuna mazao mengi, lakini watenda kazi ni wachache.
Fuatilia mahojiano haya ya ana kwa ana na Mwinjilisti Temba. Endelea;
1:Kwa nini hapa Tanzania kumekuwa na makanisa mengi, kila kukicha kuna ongezeko la makanisa?.
Mwinjilisti Temba: Ukisoma Biblia inasema, shambani mwa Bwana kuna mazao mengi. Tumuombe Bwana alete watenda kazi kwa hiyo kila kitu ninachokijibu cha Kibiblia huwa ninaangalia maandiko yanasema nini.
Ukiangalia hata watumishi tunaowaona ni wachache, makanisa mnayoyaona kulingana na Biblia bado ni machache.
Lakini,tumekuwa na hilo swali muda mrefu si nyie mmelianza ni siku nyingi sana hilo swali imeanza, zamani sana hata mwaka 1998-1990-2000 kulikuwa na maswali hayo kwa wakati ule.
Lakini, sasa nikupe jibu la msingi ni kwamba sasa hivi tupo milioni 61, hatutegemei hata Serikali inavyofanya mipango yake huduma za afya unasikia kabisa kila kata,kila kijiji umeme kila kata kila kijiji kila kitongoji.
"Sasa,Biblia inasema nyakati za mwisho maarifa yataongezeka yaani maarifa uyapate yataongezeka ina maana kuyapata unayapata kupitia watumishi.
Kwa hiyo lazima watumishi wataongezeka, waleta maarifa wataongezeka kwa hiyo kama waleta maarifa wa neno la Mungu wataongezeka ina maana idadi ya watumishi na makanisa yatakuwa mengi.
Na hoja si kuwa na makanisa mengi, hoja ni haya makanisa yanatoa nini. Hilo ndiyo jambo la msingi."
2:Sasa, kwa nini kila kanisa linalokuja linakuja na mambo yake? Mfano wengine wamekuja na maji ya upako, kwa nini?.
...Ni kweli kabisa, mimi ni mtumishi ambaye na siyo tu mafuta ya upako na maji. Mimi ndiye muhubiri wa kwanza Dar es Salaam wa kuanzisha mikesha ya usiku.
Hakuna muhubiri mwingine au kituo kingine cha redio zaidi ya Praise Power mwaka 2008 mpaka 2010 ndiyo kwanza kituo kilikuwa kinakesha.
Kipindi hicho WAPO walikuwa wanaishia saa sita, kwa hiyo mtumishi wa kwanza kukaa anaombea watu na anahubiria watu usiku kucha mimi ndiye wa kwanza.
Yaani wakati ule ambao walikuwa wanahubiriwa wakaokoka sasa hivi ni Maaskofu wakubwa sana na sitaki hata kutaja majina yao.Wako kwenye mitandao na ndiyo wanatikisa sasa hivi.
3:Kwa hiyo tunaweza kusema wewe ndiye Mwalimu wao?.
...Ndiyo, ni kama mtume tu Mungu alinipa neema kwa sababu hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa anafanya kipindi cha mkesha wa usiku.
Na wakati huo nilikuwa ninapata simu nyingi sana kwa sababu tension ya Dar es Salaam nzima, fikiria nilikuwa ninahubiri Praise Power mpaka saa tano usiku saa nyingine unashangaa.
Kumbuka nilikuwa na neema kubwa sana ya Mungu kwa sababu zile redio zinapofunguliwa hasa maeneo ya Magomeni, Manzese na Mbagala mapepo yalikuwa yanalipuka mpaka nyumba ya tano.
Kwa hiyo saa nyingine inakulazimu simu zinapoingia pale studio kulikuwa na Victor Aron. Ukimuuliza Victor Aron atakuambia wa Praise Power ilikuwa inafika muda ninasitisha mahubiri wanacheza muziki ninachukua gari yangu ninaenda Magomeni usiku saa saba kwenda kufanya delivarence na kuwaombea.
Kwa sababu kulikuwa na vitu vya ajabu, nyumba tatu...nne hadi tano kadri watu wanavyosikia ninakemea mapepo.
Watu walikuwa wanatapika, mijusi inatoka midomoni, inzi ... nini hivyo hivyo inabidi ninaenda usiku wa manane kwa sababu inashindikana, familia kule zinasema muite kwa sababu watu wanaogoba na mambo ni ya ajabu. Endelea kutazama mahojiano hapa chini;