Mwinjilisti Temba aibuka machafuko Kenya, amtaka Rais Dkt.Ruto kuwaomba msamaha Mchungaji Ezekiel na Mackenzie taifa lipone

DAR-Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amesema, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto asipowaomba msamaha Mchungaji wa Kanisa la New Life International, Ezekiel Odero na Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International waliodaiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200 nchini humo, utawala wake utarajie pigo kubwa zaidi.
Amesema, msingi wa misuguano na machafuko yanayoendelea nchini Kenya si kama wengi wanavyodhani chanzo chake ni uchumi, bali ni suala la kiroho.

Mwinjilisti Temba ameyasema hayo Julai 14,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari ambapo amefafanua kuwa,watumishi wa Mungu bila kujali udogo au ukubwa wa huduma yake wanapaswa kuheshimiwa.

"Kwanza ninataka nizungumze kuhusu Afrika Mashariki hasa kile kinachotokea kule Kenya.Nchi zetu zifike mahali ziheshimu maamuzi ya watu.

"Tatizo lililopo Kenya ni la kiroho. Watu wengi wanaona tatizo lililopo Kenya ni la kiuchumi, inawezakana kuwa la kiuchumi kutokana na namna ambavyo limeibuka, lakini msingi wa tatizo lililopo Kenya ni la kiroho.

"Moja ya shida iliyopo Kenya ni pamoja na viongozi akiwemo Rais wa Kenya mwenyewe na Mawaziri wake na baadhi ya viongozi wa chini kwenda kuwachongea wachungaji wawili walioko Mombasa kuwa wameua watu, wakati watu wale wamekufa kwenye kipindi cha UVIKO-19.
"Hivi kweli,mchungaji anaweza akaua watu zaidi ya 200 akawazika? Na wanajeshi wamo,usalama wa Taifa wamo na polisi wamo halafu wakae miaka miwili ndiyo waanze kudadavua makaburi?.

"Wamuaibishe,wamuweke jela, wamyanyase. Sasa angalia yule Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya aliyesema huyu kaua na hamtakaa mumsikie milele kafukuzwa kazi kwa aibu.

"Hii ni kwa sababu walivyoligusa na bahati mbaya viongozi wa dini wakamchochea Ruto... Paul Mackenzie na Pastor Ezekiel wamepata shida.

"Mimi nilisema awali baada ya kuulizwa kuwa hawa watu walikufa kipindi cha UVIKO-19 tangu 2020...wengi wameuliwa na UVIKO-19 kweli walikuwa kwenye maombi.

"Lakini wengi wamekufa kwa UVIKO-19 ndiyo iliyowaua. Mchungaji hawezi kuua watu wengi namna hiyo.

"Watu wakaaibisha, wakalitukana kanisa pia viongozi wa dini wa Kenya ambao walikuwa upande wa Rais wakaendelea kunyanyasa hawa watu wawili.

"Ruto uwaombe msamaha. Usipowaomba msamaha hao watu wawili hao na uwatakase mimi ninakuambia cha moto utakiona kwa sababu ni marufuku kugusa madhabau, hicho ndicho kitu wanashindwa kukielewa,"amesisitiza Mwinjilisti Temba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news