DODOMA-Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Bw. Anderson Mutatembwa ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kilichopokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Wizara za Kisekta katika eneo la Msomera na Saunyi, Tanga. Kikao hicho kilifanyika tarehe 18 Julai, 2024 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma.