DAR-Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kwa kuanzisha moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko kwa njia ya kieletroniki.

Pamoja na mambo mengine, Bi. Omolo amefahamishwa majukumu na mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu chini ya Uongozi Imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.