Naibu Katibu Mkuu,Zuhura Yunus atembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake Maonesho ya Sabasaba

DAR-Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar Es Salaam leo Julai 5, 2024.
Aidha, amehimiza watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutatua changamoto za wananchi wanaotembelea banda hilo kwa ajili ya kupata huduma na uelewa masuala yanayotekelezwa na ofisi hiyo
Katika Maonesho hayo Naibu Katibu Mkuu ametembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kujionea namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo katika maonesho hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news