DODOMA-Aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk ameandika barua ya kujiuzulu Ubunge kwa Ofisi ya Spika wa Bunge kwa kile alichoeleza kuwa anakabiliwa na changamoto za kijamii,hivyo anahitaji muda kuzishughulikia.