DAR-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo (Mb) ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini, ameongoza Kikao cha Dharura Na.1/2024 cha Baraza hilo kilichofanyika leo Julai 18, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kimejadili agenda mbalimbali ikiwemo Mikakati na Maandalizi katika kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa Mwaka 2024 na Miaka 50 ya Baraza hilo ambayo Kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Dodoma.


Tags
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
Habari
Kikao cha Dharura
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi