ZANZIBAR-Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA leo Julai 13, 2024 limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita pamoja na Ualimu nchini.
Katibu Mtendaji Mkuu wa NECTA, Dkt. Said Mohamed amesema, ufaulu wa mwaka huu 2024 umepanda mpaka asilimia 99.1.
"Katika mkutano wake wa 160 uliofanyika leo tarehe 13 Julai,2024 katika ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania zilizopo hapa Zanzibar. Baraza limeidhinisha kutangazwa rasmi kwa Matokeo ya Kitaifa ya Kidato cha Sita na Ualimu iliyofanyika mwezi Mei,mwaka huu.
"Kuhusu usajili jumla ya watahiniwa 113,536 walisajiliwa wakiwemo wanawake 50,614 sawa na asilimia 45 na wanaume 62,922 sawa na asilimia 55. Kati ya waliosajiliwa watahiniwa wa shule walikuwa 104,454 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 9,082."
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
ACSEE 2024 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES
CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET |