DAR-Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) umewataka watumishi wanaotarajiwa kustaafu kuanza kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa zao za msingi.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mafao wa NSSF Ilala, Mrisho Mwisimba wakati akimuwakilisha Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF katika warsha iliyolenga kutoa elimu kwa watumishi wanaotarajia kustaafu.
Ni kutoka katika Mkoa wa Temeke ambapo pia amewasisitiza kuanzisha miradi salama ya uwekezaji ili kuwa na uhakika wa kipato endelevu.
Kwa upande wake Emmanuel Nyange ambaye ni Meneja Idara ya Biashara wa Benki ya Biashara ya Taifa (TCB), ambao pia walihudhuria mafunzo hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha katika mafao amesema kuwa, TCB imeamua kusimama na wastaafu kwa miaka 10 sasa ikijikita katika kutatua changamoto wanazokutana nazo wastaafu.
Ni kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Kivulini isiyo na makato yeyote wala gharama za uendeshaji,lengo likiwa ni kumnusuru mstaafu
Nyange ameongeza kuwa, sambamba na hayo TCB imeanzisha huduma za pensheni advance inayomuwezesha mstaafu kupata fedha ya kujikimu kwa kutoa suluhu kwa tatizo analokutuna nalo,ila pia kuna huduma ya mkopo usio na masharti yoyote.
Aidha,kwa wastaafu watarajiwa TCB wanatoa huduma za fixed akaunti huku asilimia yake ikiwa ni mpaka 11 kwa mwaka, kupitia akaunti ya kivulini bado wastaafu wakipata majanga au ulemavu wa kudumu wanapewa fidia,na sababu kuu ni azimio la serikali kuweza kufikia makundi yote katika huduma za ujumuishaji wa kifedha.

Kwa upande wake Afisa Mafao Mkuu wa NSSF, Shakira Masoli amewasisitiza watumishi kujiandaa kustaafu kwa kuhakikisha wanapeleka na wanahakiki taarifa zote za msingi ili kuepusha usumbufu pindi wanapostaafu.
