Ofisi ya Waziri Mkuu yaibuka Mshindi wa Kwanza kwa ubora Sabasaba 2024

DAR-Ofisi ya Waziri Mkuu imebuka mshindi wa kwanza kwa banda bora na utoaji bora wa huduma kwa ngazi ya wizara zilizoshiriki katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Akipokea tuzo ya Ofisi hiyo kwa niaba ya Uongozi wa Ofisi, Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi,Bw. Condrad Millinga ameshukuru kwa namna ushindani ulivyoenda na kuipa Ofisi ya Waziri Mkuu ushindi wa Kwanza katika maonesho hayo.
Amepokea tuzo hiyo kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Sulemani Jafo hii leo Julai 13, 2024.

Maonesho hayo yamefungwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ambapo yalikuwa yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news