PPAA yaendelea kutoa elimu Maonesho ya Sabasaba

DAR-Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu mjukumu, malengo pamoja na mafanikio yake kupitia Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kupitia maonesho ya Sabasaba yanayoendelea wananchi, wazabuni, taasisi nunuzi pamoja na wadau wa sekta ya ununuzi wameendelea kupata elimu kuhusu PPAA na majukumu yake.
Mapema leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bi. Lilian Mbassy ametembelea banda la PPAA katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Bi. Mbassy amepata fursa ya kuelezewa majukumu na malengo ya Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kutoka kwa maafisa wa Mamlaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news