DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba.

Vilevile, Gavana Tutuba ameeleza kuhusu kazi za kitengo cha kupambana na utakasishaji fedha haramu na kazi zinazofanywa na Bodi ya Bima ya Amana.