Rais Dkt.Mwinyi azindua Bustani ya Mnazi Mmoja

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kutunza mazingira na kuweka haiba ya mji kuwa safi.Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Julai 15, 2024 alipofungua Bustani ya Mnazi Mmoja Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Rais Dkt. Mwinyi amesema, lengo la bustani hiyo ni kwa ajili ya mapumziko kwa wageni wanaotembelea vivutio vya utalii na wananchi wanao kwenda kuwaangalia wagonjwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza kampuni ya Infinity Development na Mamlaka ya Mji Mkongwe kwa kujenga bustani hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news