KATAVI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kufanya filamu nyingine ya Royal Tour katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kujionea wanyamapori mbalimbali katika Hifadhi hiyo.



“Tumeona mambo mengi ya kufanya mle ndani na suala la Royal Tour Waziri wa Maliasili na Utalii ameshaandika hivyo jipange na ukiwa tayari mimi mwenyewe nitakuja."
Rais Samia yupo katika ziara mkoani Katavi pamoja na mambo mengine kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo na leo ameingia mkoani Rukwa.