Rais Dkt.Samia afanya uteuzi mawaziri,Katibu Mkuu wa Madini,TRA huku Kidata akipelekwa Ikulu

NA GODFREY NNKO 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. 
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 2,2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi walioteuliwa na Rais Dkt.Samia ni Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. 

Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Dkt. Jafo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Pia,Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi huu,Mhe. Dkt. Kijaji alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Mhandisi Yahya Ismail Samamba ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini. Kabla ya uteuzi huu,Mhandisi Samamba alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. 

Mhandisi Samamba anachukua nafasi ya Bw. Kheri Abdul Mahimbali ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Bw. Yusuph Juma Mwenda ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwenda alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Bw. Alphayo Japan Kidata ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais -Ikulu. Kabla ya uteuzi huu,Bw. Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news