Rais Dkt.Samia aitaka sekta binafsi kushirikiana na Serikali kuwekeza miradi ya ubia

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wadau wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali kuwekeza katika miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public Private Partnership-PPP) hapa nchini. Miradi hiyo ni pamoja na kutengeneza vifaa vya ujenzi, kusindika mazao ya kilimo,ujenzi wa miundombinu ya barabara za tozo (Toll Roads), na ujenzi wa maeneo maalum ya viwanda (Special Industrial Zones).
Rais Samia amesema hayo leo katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) iliofanyika Ikulu.

Aidha, Rais Dkt. Samia amesema tangu kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) mwaka 2001, limeendelea kuwa chombo muhimu cha ushauri kwa Serikali kuhusu namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.
Baraza hilo limekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Sera, Sheria na Taratibu mbalimbali za biashara na uwekezaji.

Katika kufanya mageuzi na kutatua changamoto zilizobainishwa na wadau wa sekta binafsi, Rais Dkt Samia amesema kuwa Serikali itafanya tathmini ya mfumo mzima wa kodi nchini kwa lengo la kuuboresha.
Hali kadhalika, Rais Dkt. Samia amesema licha ya changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye uchumi wa dunia, uchumi wa Tanzania umekuwa himilivu, na umeendelea kukua na kuimarika zaidi.

Rais Dkt. Samia amesema hali nzuri ya kiuchumi imewezesha uchumi wa nchi kukuza biashara na kuvutia uwekezaji zaidi ambapo kati ya Julai 2021 hadi Juni 2024,Tanzania imekuwa na ongezeko la miradi ya uwekezaji 1,350 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 14.2.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news