Rais Dkt.Samia asisitiza ushirikiano kati ya Serikali na viongozi wa dini,ampongeza Askofu Pisa

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza ufanyaji kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za Dini nchini ili kuendelea kujenga amani, umoja na mshikamano.
Amesema kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizo ambao huleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

“Tunashukuru tunapata ushauri, yapo mambo ambayo mnayafanya na kuiwezesha nchi hii iendelee, mshikamano wetu ndani ya nchi, umoja wetu ndio unaozaa utulivu na amani tuliyonayo.”

Amesema hayo wakati akiwasilisha Salamu za Pongezi kutoka kwa Rais Dkt. Samia leo Jumatano, Julai 03, 2024 kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi.
Amesema kuwa, Serikali itaendelea kumpa ushirikiano wa dhati,“wakati wote utakapokuwa na jambo ambalo unadhani Serikali inahitaji kushauriwa uwe huru na wakati wote unapoona kwamba unahitaji kuunganisha nguvu na Serikali, sisi tutakupa ushirikiano.”

Ameongeza kuwa, Serikali kwa upande wake imeshaagiza ushirikiano huo usiwe tu ngazi ya kitaifa bali uende hadi katika ngazi ya vitongoji.

“Tuendelee kuwa pamoja na kuja kwangu hapa nikuhakikishie tunaendelea kukupa ushirikiano.”Kwa upande wake Askofu Pisa amemshukuru Rais Dkt. Samia Kwa salamu za pongezi za kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa TEC

Uchaguzi wa viongozi wapya wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) uliohusisha nafasi za Rais, Makamu wa Rais na Katibu ulifanyika tarehe Juni 21, mwaka huu, ambao waliochaguliwa ni Mhashamu Wolfgang Pisa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi (Rais), Mhashamu Eusebius Nzigilwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda (Makamu wa Rais) na Padre Charles Kitima Padre wa Jimbo Katoliki la Singida (Katibu Mkuu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news