Rais Dkt.Samia ataka Hospitali ya Wilaya ya Nkansi itunzwe

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka madaktari, wauguzi na watumishi wa kada zote za afya wa Hospitali ya Wilaya ya Nkansi, kuitunza miundombinu na vifaa tiba vya hospitali hiyo ambayo imekuwa ni mkombozi kwa wananchi wilayani humo.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito huo kwa watumishi hao, mara baada ya kuizindua hospitali hiyo ya Wilaya ya Nkasi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5 ikijumuisha na gharama ya vifaa tiba vilivyonunuliwa.
“Itunzeni hospitali hii yenye mindombinu bora na vifaa vipya vya kisaa kabisa, na nimeambiwa wataalam wanaovitumia vifaa tiba wamepewa mafunzo hivyo vitunzwe,” Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza.

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa, hospitali hiyo imekuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Namanyere na Wilaya nzima ya Nkansi hivyo inapaswa kutunzwa.
Aidha, amewataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa uzalendo kwa watumishi wa kada ya afya mmepewa karama na Mwenyezi Mungu ya kuokoa maisha ya watu.

“Mwenyezi Mungu amewapatia karama ya kuwa mafundi wa kutengeneza na kuokoa uhai wa mwanadamu wenzenu hivyo niwataki muifanye kazi hiyo kwa uzalendo, utaalam na weledi kwani Serikali ipo pamoja nanyi,” Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amehimiza.
Sanjari na hilo, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Namanyere na Wilaya nzima ya Nkasi kuyatunza majengo na miundombini mingine ya hospitali hiyo kwani ni mali yao na ipo kwa ajili yao.

“Haya majengo ni mali yenu yatumieni na yatunzeni ili nayo yapate kuwatunza,” Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yuko mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku 3 ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na wananchi wa mkoa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news