NA GODFREY NNKO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa mawaziri wawili na naibu waziri mmoja.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 21,2024 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
ZINAZOHUSIANA:
Mawaziri waliotenguliwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mhe. Jerry William Silaa (Mb.).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Yusuf Makamba ambaye nafasi yake imechukuliwa na Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Balozi Kombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy.
ZINAZOHUSIANA:
Vile vile, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametengua uteuzi aa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki,Mhe.Stephen Lujwahuka Byabato (Mb.) nafasi yake inachukuliwa na Mhe. Dennis Lazaro Londo.
Tags
Breaking News
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
January Yusuf Makamba
Nape Moses Nnauye
Stephen Byabato