Rais Dkt.Samia ateua tisa Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi na kumteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa tume hiyo.
Rais amefanya uteuzi huo leo Julai 31,2024 baada ya Julai 29,2024 kutangaza uamuzi wa Serikali kuunda kamati ya kutathmini na kushauri kuhusu masuala ya kodi nchini wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt.Samia amewateua pia wajumbe wa tume hiyo akiwemo Prof. Florens Luoga aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwingine ni Prof. Mussa Juma Assad ambaye alikuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Profesa Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Leonard Mususa, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PricewaterhouseCoopers (PwC) Tanzania, CPA. Aboubakar Mohamed Aboubakar , Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, Mshauri wa Masuala ya Sheria.

Wengine ni David Tarimo, Mtaalam na Mshauri wa Masuala ya Kodi na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kodi, PwC, Balozi Maimuna Kibenga Tarishi, Katibu Mkuu Mstaafu na Rished Bade, Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news