Rais Dkt.Samia atoa maagizo Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameilekeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kukamilisha Mwongozo wa Utambuzi wa Machifu na Viongozi wa Kimila katika Wilaya na Mikoa utakaoainisha majukumu yao wa kimila na kijadi.
Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo leo Julai 20,2024 wakati akizungumza na Viongozi waKimila na Machifu kutoka Tanzania nzima kwenye hafla iliyofanyika Ikulu,Chamwino.
Aidha, Rais Dkt. Samia amesema Viongozi wa Kimila na Machifu wana mchango mkubwa katika kulinda maadili na kutatua changamoto za kimaadili katika jami ili chaya kuwa yanashughulikiwa katika ngazi ya Serikali.
Rais Dkt. Samia pia ametoa rai kwa Machifu kote nchini kuendelea kujenga mvuto na uaminifu wa watu ili waweze kutoa mchango wao ipasavyo kwa ushrikiano na Serikali katika utatuzi wa migogoro inayoikabili jamii.
Vilevile, Rais Dkt. Samia amekemea vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto kwaimani potofu za ushirikina ambayo ni kinyume cha maadili ya Watanzania na kuwasihi Machifu na wananchi wote kukemea vitendo hivyo.
Vilevile, Rais Dkt. Samia ameitaka Wizara hiyo kuimarisha michezo ya Umoja wa Michezo ya Shule za Msingi na Sekondari (UMISSETA na (UMITASHUMTA) ikiwa ni sehemu ya kuwafundisha na kudumisha mila na desturi zetu.

Rais Dkt. Samia pia amesema dunia inaposhuhudia mabadiliko mbalimbali, Serikali ya Tanzania itahakikisha kuwa inashuhudia
maendeleo ambayo yanadumisha mila na desturi za Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news