Rais Dkt.Samia awaapisha mawaziri na manaibu mawaziri

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 26, 2024.
Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiapa mbele ya Rais Dkt.Samia (hayupo pichani) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Mawaziri walioapa ni Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Manaibu Mawaziri kwenye hafla hiyo.
Manaibu mawaziri walioapa ni Mhe. Deus Clement Sangu kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Dennis Lazaro Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki). Mhe. Cosato David Chumi kuwa Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news