KATAVI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wakulima kote Tanzania kwa kiwango cha uzalishaji wa chakula na kuifanya nchi kuwa na utoshelevu wa chakula unaozidi asilimia 120.


Vile vile, Rais Dkt. Samia amezitaka halmashauri zote katika Mkoa wa Katavi kuacha tabia ya kuwatoza wananchi ushuru wa mazao kwa kiasi kisichozidi tani moja na kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali hapo awali.