Rais Dkt.Samia azindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo,atoa maagizo

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kutumia jengo jipya la halmashauri kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito huo kwa watumishi wa halmashauri hiyo, wakati akiongea na wananchi wa Kalambo mara baada ya kulizindua jengo hilo la kisasa.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema, jengo hilo linatumiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri na watumishi wa Idara zote ambao watakua wanatoa huduma kwa wananchi ndani ya jengo moja.

“Jengo hili litarahisha uratibu wa shughuli za halmashauri na utoaji wa huduma kwa wananchi, hivyo niwaombe watumishi mtakaolitumia mtimize wajibu wenu kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi ambao ndio wajiri wetu,” Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza kuwa, Serikali yake imeboresha mazingira ya kufanya kazi kwa watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa kujenga jengo zuri la halmashauri, hivyo anatarajia watalitumia kutatua changamoto zote zinazowakabili wananchi.

Aidha, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewahaidi wananchi wa Kalambo kuwa, Serikali yake itaendelea kuijenga hamashauri yao kwa kuendelea kufanyia kazi changamoto zote zinazowakabili.
Leo ni siku ya pili ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Rukwa, ambapo ameitembelea Wilaya ya Kalambo na kuzingua Jengo la Halmashauri hiyo lililojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news