DAR-Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi amewasili nchini leo Julai 1, 2024 kwa ziara ya Kitaifa hadi Julai 4, 2024 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Nyusi amepokelewa na viongozi waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba.
Hata hivyo,mapokezi rasmi ya kiongozi huyo wa Msumbiji yatafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kesho Julai 2, 2024.